Katibu mkuu wa Azam fc amesema kuwa msafara wa azam fc unao kwenda Sudani kusini siku ya jumamosi machi 2 kwa ajili ya mchezo wa marejeano wa kombe la shirikisho utakuwa na watu 27, ambapo wachezaji watakuwa 20 na viongozi 7.
Nassoro aliongeza kuwa mchezo huo wanataraji utakuwa mgumu kwao kwa kuwa wapinzani wao Al-nasri pamoja na wao wana nia ya kusongo mbele kwa hatua inayofuata.
Katika mchezo wa awali uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam azam fc walishinda kwa goli 3-1 hivyo kuhitaji sare yoyote katika mchezo huo utakaochezwa jumapili machi 3 ama wasiruhu kufungwa tofauti ya magoli zaidi ya 2 ili kusonga mbele.
Katika hatua nyingine uongozi wa azam fc umetuma maombi kwa shirikisho la soka nchini TFF limruhusu kukaa kwenye benchi a azam kocha wao msaidizi Kally Ongala wakati wanaendelea kuchunguza vyeti vyake.
Ongala aliziuiwa na TFF kukaa kwenye benchi la azam mpaka watakapo maliza kupitia vyeti vyake vilivyowasilishwa katika ofisi za TFF.
Katibu mkuu wa azam fc Nassoro Idrissa alisema kuwa wameamua kuiandikia barua ya kuwaomba TFF wamruhusu Ongala kukaa kwenye benchi wakati uchunguzi juu ya vyeti vyake ukiendelea.
"Ongala alifungiwa lakini tulishapeleka vyeti vyake muda mrefu lakini mpaka sasa wamekaa kimya hivyo tumewaandikia barua ya kumruhusu kocha huyo msaidizi mpaka pale watakapojiridhisha na uchunguzi wao," alisema Nassoro Idrissa.
Uongozi wa azam fc wamefikia hatua hiyo baada ya kocha wao mkuu Stewart Hall kufungiwa kwa michezo mitatu ya ligi kuu ya vodacom pamoja na kutozwa faini ya Tsh 500000 kwa kosa ya kutooa bukta yake katiki mchezo dhidi ya Kagera sugar uliochezwa katika uwanja wa azam complex.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment