AZAM WAANZA NA USHINDI CAF

Azam fc leo wameanza na ushindi katika michuano ya kombe la shirikisho (CAF Confideration cup) baada ya kuwachapa goli 3-1 Al-Nasri JUba mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Azam fc kama ada yao kuhakikisha kupata goli katika dakika ya 20 ambapo dakika ya 14 Abdi Kassim Babi aliifungi. azam fc goli la kuongoza akiunga mpira wa Kipre Tchetche.

Baada ya goli hilo kuingia azam waliendelea kulisakama lango la al-nasri na katika dakika ya 16 Brian Umonyi alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Khamis Mcha.

Katika dakika ya 28 Michael Bolou aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Jabir Azizi. na katika dakika ya 38 al-nasri wal4rwawazisha goli hilo kupitia kwa Fabian Alies na kupelekea timu kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.

Kipindi cha pili azam waliuwanza mchezo kwa kasi na kupoteza nafasi kazaa kupitia kwa Abdi Kasim na katika dakika ya 62 Abdi Kasim alienda benchi na nafasi yake kujazwa na John Bocco ambaye aliingia kwa kasi na kukosa nafasi ya goli.

Katika dakika ya 79 Kipre Herman Tchetche aliandika goli la pili kwa azam fc akimalizia kwa kichwa kazi nzuri ya Khamisi Mcha Viali goli lilizidisha hamasa kwa azam ya kusaka goli 3.

Alikuwa John Raphael Bocco aliyehitimisha kalamu ya magoli kwa kuifungia goli la 3 azam fc katika dakika ya 90 na kupelekea mchezo kumalizika kwa azam kushinda goli 3-1.

Azam na al nasri watarejeani kati ya machi 1-3 katika mji wa Juba Sudan kusini.

azam leo; MWADINI ALLY, HIMID MAO, MALIKA NDEULE, DAVID, JOACKINS ATUDO, MICHAEL BOLOU/JABIR AZIZI, SALUM ABOUBAKARY, HAMPHREY MIENO, ABDI KASIM / JOHN BOCCO, BRIAN UMONY /JHAMISI MCHA, KIPRE TCHETCHE



--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.