AZAM WAENDELEZA KICHAPO, WATOKA BILA NYAVU ZAO KUGUSWA

Kwa mara ya kwanza toka mzunguko wa pili mabingwa wa kombe la mapinduzi azam fc wanamaliza dakika 90 bila ya nyavu zao kuguswa huku wakitoa dozi ya goli 4 kwa jkt ruvu.

Azam fc leo walikuwa wageni wa jkt ruvu katika uwanja wa azam complex katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ambapo azam fc wamefikisha point 36 baada ya kushinda leo wakizidiwa na yanga tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa 4 wakiwa sawa katika point.

Katika mchezo huo wa leo azam fc waliuwanza kwa kasi mchezo huo na kama ilivyoada katika dakika ya 3 Khamisi Mcha Viali aliiandikia goli la kuongoza azam fc na kupelekea kuwaamsha JKT ruvu na kuanza kushambulia lango la azam.

JKT Ruvu walipata penati ambayo waliikosa na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga kitendo kilichopelekea kutoka bila goli hii leo.

John Bocco aliifungia azam fc goki la pili wakati timu zikijianda kwenda mapumziko katika dakika 45 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Shaban Dihile na kuipeleka mapumziko azam wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Utamaduni wa kufunga katika dakika 20 za mwanzo za kila kipindh uliendelea kufuatia goli la Khamisi Mcha katika dakika 46 na kuipa uongozi wa goli 3-0 azam fc.

Azam fc waliwapumzisha Kipre Tchetche na John Bocco na nafasi zao kuchukuliwa na Seif Abdallah na Abdi Kasim Babi kabla ya Mwaikimba kuchukua nafasi ya Mwaipopo.

Abdi Kasim akigusa mpira wake wa kwanza aliipatia azam goli la 4 katika dakika ya 74 na kupelekea mchezo kumalizika kwa azam kushinda goli 4-0.

AZAM FC LEO
MWADINI ALLY
HIMID MAO
WAZIRI SALUM
JOACKINS ATUDO
DAUD MWASINDIKE
JABIR AZIZI
KIPRE TCHETCHE/ABDALLAH SEIF
IBRAHIM MWAIPOPO/GAUDENCE MWAIKIMBA
JOHN BOCCO/ABDI KASIM
HUMPHREY MENO
KHAMISI MCHA


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.