AZAM WAITUNGUA 4 MTIBWA WAIKAMATA YANGA

Ligi kuu ya vodacom imeendelea leo kwa mchezo mmoja uliochezwa katika uwanja wa Manungu complex mkoani Morogoro kwa kuwakutanisha mtibwa sugar na azam fc.

Azam fc ambayo huinyanyasa mtibwa sugar katika uwanja wa manungu leo wamerejesha rikodi yao ya kuwachapa mtibwa sugar goli 4 katika uwanja huo kikiwa ndicho kipigo kikubwa kukipata mtibwa katika uwanja wake wa manungu..

Ushindi huo wa goli 4 umeifanya azam fc kuikamata yanga kwa kufikisha point 33 sawa na yanga yenye point 33 wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Kama ilivyo ada kwa azam fc kuhakikisha ndani ya dakika 15 za kipindi cha kwanza wanakuwa teyari wamespata bao toka duru la pili lianze, ndicho kilichotokea manungu leo baada ya beki Joacsan Atudn kuiandikia azam goli la kuongoza katika dakika ya 14 akiunga mpira wa Abdi Kassim.

Katika dakika ya 21 mtibwa sugar walitumia makosa ya mabeki wa azam kupata goli la kufutia machozi kupitia kwa mchezaji wa zamani wa yanga na kagera sugar Vicent Barnabas.

Kuingia kwa goli hilo la mtibwa kulipelekea timu hizo kushambuliana kwa zamu na kipindi cha kwanza kikimalizika kwa sare ya goli 1-1.

Kilicho imaliza toto africa pale chamanzi ndicho kilicho mmaliza mtibwa sugar hii leo katika uwanja wake wa manungu, si wengine bali ni Brian Umony na Humphrey Meno, ambapo kama ilivyoada wal4ongeana pasi na Umony kvia mpira kimiani katika dakika ya 46 na kuiandikia azam goli la 2.

Mtibwa sugar walicharula na kuanza kuliamdama lbngo la azam bila majibu ndipo mtokea benchi akicheza kwa mara ya kwanza katika duru la pili Kipre Herman Tchetche kuhitimisha kalamu ya magoli kwa kuifun4a azama goli la 3 na la 4 katika dakika ya 89 na 90.


Na kupelekea mchezo kwisha kwa ayam eckthbgpa gokh 4 kwa 1 la mtibwa sugar.



[MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA MATATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com]

Hizi ndizo point zilizo vunwa na kila timu na michezo iliyocheza:

1. YANGA SC 15 33
2. AZAM FC 16 33
3. SIMBA SC 16 28
4. COASTAL UNION 16 27
5.KAGERA SUGAR 16 26
6. RUVU SHOOTING 15 24
7. MTIBWA SUGAR 16 23
8. JKT OLJORO 16 21
9. PRISONS 16 19
10. MGAMBO SHOOTING 16 18
11. JKT RUVU 15 16
12. TOTO AFRICA 16 13
13. POLISI MORO 15 10
14. AFRICAN LYON 16 9


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.