BASI LA BAUSI LASHINDIKANA, APIGWA 4

Kocha wa African lyon Salum Bausi jana alijinadi leo atahakikisha timu yake inalazimisha suluhu katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom dhidi ya yanga uliochezwa katika uwanja wa taifa.

Katika mchezo wa leo African lyon waliingia wakiwa na dhamira ya kuzuia wasifungwe goli hata moja na yanga kwa kiswahili maarufu cha watu wa mpira walikuwa na dhamira ya kupaki basi lakini walijikuta wakitota na basi lao kwa kufungwa goli 4-0.

Yanga ambao walitawala vilivyo mchezo walianza kuandika goli la kuongoza katika dakika 21 kupitia kwa alipata kuwa mshambuliaji wa taifa stars Jerry Tegete na alirejea tena kwenye nyavu za lyon katika dakika 42 na kuitoa yanga mapumziko wakiwa wanaongoza goli 2-0.

Katika kipindi cha pili wakicheza kama wako mazoezini yanga walipata penati katika dakika 48 na Hamisi Kiiza akaipoteza penati hiyo.

Didier Kavumbagu akitokea benchi kuchukua nafasi ya Jerry Tegete aliiandikia yanga goli la 3 kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 70, ikiwa kabla ya Nizar Khalfan aliyechukuwa nafasi Saimon Msuva kuhitimisha kalamu ya magoli katika dakika ya 80 akiiandikia yanga goli la 4.

Kwa matokeo hayo ya leo Yanga imejikita kileleni kwa kufikisha point 36 waki wazidi Azam fc point 3, huku lyon wakijiweka katika nafasi mbaya ya kusalia ligi kuu kwa kupuruza mkia (kuwa wa mwisho).

--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.