BAUSI AANZA NA MBILI MBEYA, MOROCO ABANWA MWANZA

Makocha toka visiwani Zanzibar, Hemedi Moroco na Salum Bausi leo wameshindwa kukusanya point zote 3 katika mikoa ya Mwanza na Mbeya ambayo timu zao za Costal union na African lyon walikuwa wanacheza mchezo wao wa 16 wa ligi kuu ya vodacom.


SOKOINE MBEYA

Katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Prisons iliwakaribisha vijana wa Bausi African lyon na mchezo ukimalizika kwa kushuhudia kocha anaetembea kwenye kauli zake Bausi akianza kibarua chake kipya kwa kufungwa goli 2-0 na prisons.

Katika mchezo huo Prisons waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 9 kupitia kwa Elias Maguli kabla Sino Agustino kukamilisha kalamu ya magoli kwa kuifungia prisons goli la pili.


KAITABA, KAGERA

Katika uwanja wa Kaitaba wenyeji Kagera sugar waliwakaribisha Mgambo shooting na mchezo kwisha kwa Kagera sugar kushinda goli 1-0.

Kagera sugar iliyopoteza michezo miwili ya mwanzo ya ugenini na leo katika uwanja wake wa nyumbani wameshinda goli 1-0 goli hilo ilifungwa na Julius Mrope.


CCM KIRUMBA, MWANZA

Baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo katika majiji ya Arusha na Dar es salaam, Toto Africa wamelazimishwa sare na Coastal union katika uwanja wake wa nyumbani.

Toto Africa leo waliutawala mchezo kwa kiasi kikubwa na kupoteza nafasi nyingi za kufunga.


[MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA MATATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com]

Hizi ndizo point zilizo vunwa na kila timu na michezo iliyocheza:

1. YANGA SC 15 33
2. AZAM FC 15 30
3. SIMBA SC 16 28
4. COASTAL UNION 16 27
5.KAGERA SUGAR 16 26
6. RUVU SHOOTING 15 24
7. MTIBWA SUGAR 1523
8. JKT OLJORO 16 21
9. PRISONS 16 19
10. MGAMBO SHOOTING 16 18
11. JKT RUVU 15 16
12. TOTO AFRICA 16 13
13. POLISI MORO 15 10
14. AFRICAN LYON 16 9

--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.