BAUSI ACHUKUA KAZI YA MUARGENTINA

Aliyekuwa kocha wa Zanzibar heroes mwaka jana katika michuano ya Tusker chalenge cup iliyofanyika nchini Uganda, Salum Bausi amechukuwa nafasi ya Muargentina Pablo Ignacio Velez katika timu ya African lyon na kufikisha idadi ya makocha wawili toka visiwa vya karafuu Zanzibar kufundisha timu za ligi kuu msimu huu (2012/13).

Bausi aliyeiwezesha Zanzibar heroes kushika nafasi ya 3 katika michuano ya tusker chalenge alianza kazi yake mpya ya kuhakikisha African lyon inasalia kwenye ligi hapo jana na mchezo wake wa kwanza utakuwa ugenini Mbeya kuwakabili Prisons ya mkoani huko.

Lyon imeuwanza vibaya mzunguko wa pili na kupelea kuburuza mkia katika msimamo wa ligi kuu baada ya kupoteza michezo miwili ya mwanzo ya duru hili la pili.

Bausi na Hemedi Moroco anae fundisha coastal union ya Tanga ndio Wanzanzibari pekee waliopewa jukumu la kuongoza vikosi viwili kati ya 14 vinavyo shiriki ligi kuu ya vodacom 2012/2013.

--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.