Coastal union walianzia Mwanza jumamosi na kutoka sare ya bila kufungana na Toto Africa kabla ya kusafiri kuelekea Kagera kuwakabili wakatamiwa wa huko mchezo uliochezwa leo katika uwanja wa kaitaba.
Katika mchezo huo wa leo Coastal union walikubali kulala kwa goli moja bila mbele ya Kagera sugar goli likifungwa na Themi Felixs katika dakika ya 58, na kuipelekea coastal kuambulia point moja katika ziara yake ya kanda ya ziwa.
Katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya vodacom ulhchezwa katika uwanja wa mkwakwani kwa kuwakutanisha Mgambo JKT na JKT Oljoro na mchezo kwiqha kwa oljoro kufungwa goli 2-0.
Magoli ya ushindi ya Mgambo shoothng yalifungwa na Nassoro Gumbo akifunga katika kila kipindi
Wakati huo huo Toto Africa wameambulia sare ya kufungana goli 2-2 na polisi moro katika mchezo uliochezwa CCM Kirumba.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment