JAMHURI WAPIGWA, SIMBA LEO TAIFA

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa Afrika Jamhuri ya Pemba jana wamepokea kichapo wakati wawakilishi wengine katika michuano hiyo Simba sc wanataraji kucheza leo katika uwanja wa taifa.

Jamhuri jana jioni waliwakaribisha ST.George ya Ethiopia katika uwanja wa Gombani katika kisiwa cha Pemba na kushuhudia Jamhuri wakilala kwa goli 3-0 mbele ya mashabili wao waliojiokeza kuwapa sapoti.


Simba sc wao watakuwa wanawakaribisha Lupopo ya Angola katika uwanja wa taifa mchezo utakao anza mishale ya saa kumi alasiri.

Simba sc watateremka na kikosi chake chote huku beki wa kikosi hiko Shomari Kapombe akiwataka mashabiki wa simba wasiwe na mashaka na timu yao huku msemaji wa timu hiyo Ezekile akisema wanamatumaini ya kufanya vyema.

Ezekile amesema kuwa michuano ya kimataifa ni tofauti na ligi kuu ya vodacom hivyo ni mataumaini yao kesho kushinda ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutinga katika hatua inayo fuata.


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.