KAPOMBE AINYIMA USHINDI SIMBA

Beki wa kimataifa wa Tanzania anaekipiga Simba sc Shomari Kapombe ameinyima timu yake ushindi hii leo, katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochfzwa Taifa baada ya kukosa mkwaju wa penati uliopatikana katika dakika ya 89.

katika mchezo huo ambao ulishuhudia mshambukiaji wa zamani wa simba Mussa Hassan Mgosi akirejea katika ligi kuu ya vodacom baada ya kuwa DR Congo na aliporejea nchini alijiunga na JKT Ruvu mwanzoni mwa msimu hu na alikaribia kutikisa nyavu za simba katika dakika ya 8 ya mchezo baada ya kubaki yeye na Kaseja na mpira alioupiga ukatoka nnje.

Katia dakika ya 18 Abdallah Seseme alipiga mpira ukatemwa na kipa Shaban Dhhile na kumkuta Amir Kiemba aliyeifungia simba goli la kuongoza na kuipeleka simba wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Katika kipindi cha pili jkt ruvu walionyesha dhamira ya kutafuta goli la kusawazisha huku simba wakisaka golh la ushindi.

Katika dakika ya 62 shuti la mbali la Johnson Malali lilitinga nyavuni kwa simba na kupelekea ubao kusomeka 1-1.

Wakati mpira ukielekea kwisha amanusura simba wapate goli la ushindi baada ya kupata penati katika dakika ya 88 na Kapomae akakosa penati hiyo na kupelekea mchezo kumalizika kwa rare ya goli 1-1.


Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo uliochezwa katika uwanja wa mkwakwani Tanga na kuwakutanisha coastal union na prirons ulimalimalizika kwa sare ya bila kufungana (0-0)


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.