Simba na Prisons wanakutana katika uwanja wa Sokoine ambapo mara ya mwisho timu hizo kukutana katika uwanja huo ilikuwa msimu wa 2008/2009 ambapo simba sc kwa mara ya kwanza walifanikiwa kuchukua point zote 3 na mwisho wa msimu prisons ikashuka daraja.
Simba inakutana na prisons katika uwanja wenye rikodi mbaya kwao wakiwa wamecheza michezo mitatu ya ligi kuu na kufanikiwa kuchukuwa point 5 katika michezo hiyo kabla ya kufungwa na Libolo hapo jumapili katika uwanja wa taifa katika mchezo wa klabu bingwa Afrika.
Hayo ni matokeo mabaya kwa simba huku mashabiki wakianza kutokwa na imani na uwongozi wa simba kwa kushindwa kuchukua point zote 9 katika michezo 3.
Prisons imetoa sare na timu zote zilizo kwenye mbio za ubingwa msimu katika uwanja wa Sokoine ambapo walitoka sare ya bila kufungana na Yanga na Azam, hivyo kupelekea mchezo huo kuwa mgumu kwa simba.
[MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO LA COMPUTER YAKO.
TUPO MANYARA (MIKOVILA) MIKOCHENI B
Tupigie 0657184421 ]
Simba imeenda jijini Mbeya bila ya wachezaji wake watano ambao ni Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Paul Ngalema na Edward Christopher walio majeruhi, wakati Mussa Muddde akiwa amerejea nchini Uganda kushirhki msiba wa mwanae.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment