Katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom simba walipata goli pekee la ushindi kupitia kwa Kiemba katika kipindi cha kwanza cha mchezo goli lililodumu dakika zote 90 za mchezo.
Ushindi huo uliopelekea simba kufikisha point 31 ni ushindi wapili kwa simba katika michezo 4 ya ligi kuu ya vodacom waliyocheza katika duru hili la pili, wakiwa wametokea kupokea kichapo cha goli 1-0 toka kwa Libolo katika michuano ya klabu bingwa Afrika.
Ushindi huo vile vile ni wapili mfululizo kwa simba katika uwanja wa Sokoine ambapo msimu wa 2008/09 ndio ulikuwa msimu wa mwisho kwa simba kucheza mchezo wa ligi katika uwanja huo baada ya kuwachapa prisons na prisons kushuka daraja na msimu huu wa 2012/13 ndipo wakarejea ligi kuu ya vodacom na kukumbana na kichapo hicho cha goli 1-0 toka kwa simba.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment