Katika mchezo huo yanga na Mtibwa sugar waliuwanza kwa kushambuliana kwa zamu huku Vicent Barnabas, Rashid Gumbo, Shaban Kisiga na Husein Javu walikuwa mwiba kwa yanga wakati Kavumbagu na Athuman Iddi Chuji mchezo ukiwakataa.
Katika dakika ya 44 Idrisa Rashid Baba ubaya aliamba na mpira pembeni na kupiga krosi ambayo amanusura Mtibwa sugar wapate bao kama washambuliaji wake wangekuwa teyari wameshafika katika 6 ya yanga na mpira kwenda upande wa pilh uliko mkuta Mkopi na alipojaribu kurejesha kati ulimgusa mchezaji wa yanga na kuzaa kona iliyo pigwa na Issa Rashid na kuungwa na Shaban Kisiga na kuzaa goli la kuongoza kwa mtibwa katika dakika ya 45
Katika kipindi cha pili yanga walianza na kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Kavumbagu na Chuji na nafasi zao kuchukuliwa na Nurdin Bakari na Hamisi Kiiza mabadiliko yaliyorejesha mchezo kwa upande wa yanga.
Mwanzoni mwa kipindi cha pili mtibwa amanusura wapate goli la pili baada ya shuti la mchezaji wa mtibwa kugonga mwamba.
Yanga walimpumzisha Franky Domayo na kumuingiza Said Bahamuzi huku mtibwa wakiwatoa Ally Mohamed Gaucho, Barnabar na nafasi zao kuchukuliwa na Babu Ally na Jamal Mnyate, mabadiliko yaliyopelekea yanga kuliandama lango la mtibwa sugar.
Katika dakika ya 86 yanga nusura wapate goli baada ya Jerry Tegete kuutoa nnje mpira pake alipo baki na kipa wa mtibwa sugar.
Alikuwa Kiiza aliyeizawadia yanga point moja leo kwa kufunga goli la kusawazisha katika dakika ya 87 na kuifanya yanga kufikisha point 30.
Mpaka mpira unakwisha yanga goli moja na mtibwa moja na kupunguza tofauti ya point baina ya azam na yanga kuwa 3 badala ya 5 kama wange shinda leo.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment