KMKM WAJIKITA KILELE ZGPL

Ligi kuu ya Zanzibar grand malt (ZGPL) imeendelea leo kwa michezo miwili ambayo ilichezwa katika visiwa vya Pemba na Unguja na kushuhudia mabaharia wa KMKM wakizidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

KMKM jioni ya leo walikuwa na kibarua na bandari fc katika uwanja wa Amani uliopo katika kisiwa cha Unguja na KMKM kufanikiwa kuondoka na ushindi wa goli 1-0.

Goli hilo la ushindi kwa kmkm lilifungwa na Khamisi Simba na kuipa ushindi timu yake ya KMKM wa goli moja bila.
.

Mchezo mwingine wa ligi hiyo ulichezwa katika uwanja wa Gombani uliopo katika kisiwa cha Pemba kwa kuwakutanisha wawakilishi wa Zanzibar katika klabu bingwa Afrika Jamhuri dhidi ya mabingwa wa ligi hiyo Super falcon.

Katika mchezo huo jamhuri iliyotokea katika kupokea kichapo cha goli 3 toka kwa St. George ya Ethiopia katika michuano ya klabu bingwa na leo kuzinduka na kuwachapa super falcom goli 1-0.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.