KMKM WATOA SULUHU, MUNDU WATOA SARE

Ligi kuu ya Zanzibar Grand malt imeendelea leo kwa michezo miwili katika mji wa Pemba na Unguja na kushuhudia sare katika michezo yote.

Katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba kulikuwa na mtanange kati ya Duma na Falcon na kushuhudia mchezo ukimalizika kwa sare ya goli 1-1.

Super falcon walikuwa wa mwanzo kupata goli katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Omary Ahmed, goli lililo waamsha Duma na kuanza kuliandama goli la falcon lakini mpaka timu zinakwenda mapumziko falcon walikuwa mbele kwa goli 1-0.

Katika kipindi cha pili duma waliendelea kulisakama lango la falcon na katika dakika ya 62 Mohamed Salim aliipatia duma goli la kusawazisha kwa kuunga mpira uliotemwa na kipa wa falcon kufuatia mpira wa kona na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.


Katika kisiwa cha Unguja kulishuhudia mchezo kati ya MALINDI na KMKM uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.

--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.