LYON WAIOTEA TOTO

Ligi kuu ya vodacom iliendelea leo katika uwanja wa CCM Kirumba kwa Toto Africa kuwakaribisha African lyon na kushuhudia jahazi la Toto likielekea kuzama wakati la lyon likianza kuchungulia kutoka katika kuzama.

Katika mchezo huo lyon walifanikiwa kuwafunga goli 2-0 toto afrika ukiwa ndio ushindi wake wa kwanza toka duru la pili lianze na kufikisha point 12.

Lyon waliliona lango la Toto Afrika katika dakika ya 20 kupitia kwa Fredy Lewis na kuipelekea lyon kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilikuwa ni cha kutawala kwa kupokezana na kwa makosa ya mabeki wa Toto kulipelekea lyon kuandika goli la pili kupitia kwa Benedict katika dakika ya 89.

Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa wana Mbagala African lyon kuji9olea point zote 3 katika uwanja mgumu kuchukua point zote na magoli mawili mbele ya TOTO African ya jiji hilo la miamba ya mawe Mwanza.



--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.