MTIBWA HALI MBAYA MANUNGU, POLISI WAENDELEA KUZINDUKA

Mabingwa wa Tanzania bara katika mwaka 2000 na 1999 Mtibwa sugar wameendelea kufanya vibaya katika michezo yake ya uwanja wa nyumbani Manungu complex baada ya kuambulia pointi 1 hii leo.

Mtibwa sugar waliwakaribisha Tanzania prinsons ya Mbeya katika uwanja wake wa Manungu complex nna mchezo kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Toka duru la pili lianze mtibwa sugar bado hawajapata ushindi katika uwanja wake wa Manungu wakiwa wameteremka mara 4 katika uwanja huo katika duru la pili.


Mchezo mwingine wa ligi kuu ya vodacom ulipigwa katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro mjini kwa kuwakutanisha Polisi morogoro na mgambo shooting.

Katika mchezo huo ulimalizika kwa Polisi morogoro kuibuka na ushindi wa goli 1-0 goli lililo fungwa na Nahodha Salum.

Ushindi huo unaibakisha polisi moro katika nafasi ya 13 kwa kufikisha point 15 wakiwa mbele kwa point 3 dhidi ya African lyon anaeshika nafasi ya mwisho kwa kuwa na point 12 na wakiwa nyuma kwa point 1 dhidi ya Toto Africa na JKT Ruvu.


Ligi hiyo itaendelea kesho katika uwanja wa azam uliopo Chamanzi kwa kuwakutanisha JKT Ruvu na Toto Africa.


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.