Coastal union inayoshika nafasi ya 4 leo waliwakaribisha ruvu shooting inayo fundishwa na Charles Mkwasa katika uwanja wa CCM Mkwakwani na mchezo huo kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
Kwa matokeo hayo coastak union wamefikisha point 31 sawa na simba sc lakini wakizidia katika uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa na kuwafanya wabakie katika nafash ya 4 na simba kuendekea kukalia nafasi ya 3.
[TATIZO LA COMPUTER YAKO LITATATULIWA NA MSUNI CNMPUTER SOLUTION
www.aboodmsuni21.blogspot.com ]
Katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa taifa ulishuhudia yanga wakichomoka na pointi zote tatu kupitia kwa kiungo wao toka Rwanda Haruna Niyonzima aliyeipatia yanga goli pekee na kuendelea kuiacha azam fc kwa point 6 na kujikita kileleni.
Katika mchezo huo dhidi ya Kagera sugar kocha wa yanga aliwanzirha Didier Kavumbagu na Said Bahanuzi katika safu ya ushambuliajh na mpaka wanakwenda mapumziko hamna timu iliyo ona lango la mwenzake.
Katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza nusura yanga waandike goli la kwanza kupitia kwa Kavumbagu kwa mkwaju wa penti ambayo Kavumbagu aliikosa.
Yanga walipata goli la kuongoza na la ushindi kupitia kwa aliyeiangamiza azam fc Haruna Niyonzima aliyeachia shuti kali lililo mshinda mlinda lango wa kagera sugar katika dakika ya 66.
Katika dakika ya 70 Kavumbagu na Bahamuzi waliwapisha Jerry Tegete na Hamisi Kiiza mabadiliko ambayo hayakuathiri matokeo ya mchezo huo.
Kwa matokeo ya leo yanga wamefikisha point 42 wakiwa na michezo sb na azam fc yenye point 36 wakishika nafasi ya pili wakati yanga wakiongoza msimamo wa ligi.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment