Msafara wa simba sc utaongozwa na Zakaria Hans Pope ikiwa na wachezaji 18 pamoja na viongozi 7 na utaanza safari ya kuelekea Luanda Angola saa 11 alfajiri, wakiondoka na shirika la ndege la Kenya.
Simba sc watacheza na Lubolo siku ya jumapili machi 3, ambapo simba sc wanatakiwa wapate ushindi wa goli 2-0 kama kweli wanahitaji kutinga katika hatua ya awali ya klabu bingwa Afrika.
Katika mchezo wa awali uliochezwa katika uwanja wa taifa ulishuhudia simba sc wakilala goli 1-0 toka kwa Libolo.
Wachezaji watakao ondoka kesho ni:
JUMA KASEJA, ABBEL DHAIRA, NASSOR SAID CHOLO, AMIR MAFTAH, JUMA NYOSO, SHOMARI KAPOMBE, KOMABIL KEITA, SALIM KINJE, KIGGI MAKASY, AMIR KIEMBA, MWINYI KAZIMOTO, HARUNA MOSHI BOBAN, MRISHO NGASSA, RAMADHANI CHOMBO, ABDALLAH SESEME, HARUNA CHANONGO NA ABDALLAH JUMA.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment