Watu wa mpira husema mpira ni dakika 90, dakika 90 ndizo zinazotoa majibu ya nani wa kucheka na nani wa kununa, ila kuna vitu vinavyoweza kupelekea kubashiri matokeo ya mchezo husika, ambayo yana nipelekea kusema kuwa simba sc msimu huu wa 2012/13 hana chake kukiwa kumebakia michezo 8 msimu kumalizika.
Michezo 8 ni mingi kubadilisha msimamo wa ligi hususani pale unapo ona wajuu yako unapishana nae pointi 5 na anaeongoza ligi unapishana nae kwa pointi 8 huku wachini yako anaweza kukuvuta shati kwa kuwa unapishana nae kwa point 1.
Ila kwa simba msimu huu kusogea mbele (kushika nafasi ya 2) ama kwenda kwenye uongozi ni kitu cha kufikirika kwenye ndoto kutokana na ratiba ya michezo iliyo salia inaonyesha simba ina michezo migumu 5, wakati yanga ikiwa na michezo migumu 2 na azam wakiwa nayo 2.
Simba sc inaweza michezo yote 8 ikawa migumu kutokana na kuwa na wakati mgumu pindi anapo kutana na timu za jeshi katika mzunguko huu wa pili ambapo katika michezo 3 dhidi ya jkt ruvu, jkt oljoro na prisons wamefanikiwa kupata point 5 wakifunga magoli 3.
Simba wamebakisha dhidi ya majeda watatu ambao wote wako katika hali ya kujiweka katika mazingira mazuri ya kutokamatwa na walio chini yake ambao ni polisi morogoro, mgamba shooting, na ruvu shooting zote zikichezwa katika uwanja wa taifa, na simba wanaweza wakachukuwa point zote 9 kama watabadilika kwa kuyafanzia kazi mapungufu yao.
Simba sc inasafari ya kwenda katika vhwanja ambavyo hawatamani kuvisikia kwa kuwa na rikodi mbaya navyo ambavyo ni ccm kirumba Mwan9a na kaitaba Kagera ambapo watacheza na kagera sugar na toto africa katika michezo mitano migumu waliyobakiwa nayo.
Michezo mingine migumu ni dgdi ya mpinzani wake wa jadi yanga, anae gombania nae katika nafasi ya 2 azam na anae chuana nae katika nafasi ya 3 coastal union, michezo yote itachezwa katika uwanja wa taifa.
Ni ndoto ambayo kila shabiki wa simba anaota kwa simba kuchukua point z6te 15 katika michezo hiyo 5 ambayo naiangalia simba kupoteza point si chini ya 5.
Nte ya hapo simba watakuwa na mtihani pale watakapo cheza na coastal katika uwanja wa taifa siku 3 mbele wanatakiwa kuwa Kagera kuwakabili kagera sugar.
Kwa haraka haraka simba hii hatakuwa ajabu kukamata nafash ya 5 mwishoni mwa msimu wakati itakuwa ni maajabu kwa simba hii kushika nafasi ya 2.
[ MSUNI COMPUTER SOLUTION
NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blngspot.com ]
RATIBA YA MICHEZO ILIYOSALIA KWA YANGA, AZAM NA SIMBA
YANGA
(kiporo) yanga vs jkt ruvu, u/taifa
09/3 yanga vs toto africa, u/taifa
27/2 yanga vs kagera, u/taifa
:16/3 ruvu shooting vs yanga, u/taifa
30/3 polisi moro vs yanga, jamhuri
13/4 mgambo shooting vs yanga, ccm mkwakwani
10/4 yanga vs oljoro, u/taifa
1/5 yanga vs coastal union, u/taifa
18/5 yanga vs simba, u/taifa
AZAM FC
9/3 azam vs african lyon, u/azam comp
13/3 azam vs polisi morogoro, u/azam comp
16/03 azam vs prisons, u/azam comp
30/3 ruvu shooting vs azam, mabatini
13/4 azam vs simba, u/taifa
27/4 coastal union vs azam, ccm mkwakwani
11/5 azam vs mgambo shooting, u/azam comp
18/5 oljoro vs azam, sh.amri abeid
SIMBA SC
09/3 ruvu shooting vs simba, u/taifa
13/3 simba vs coastal union, u/taifa
16/3 kagera sugar vs simba, kaitaba
30/3 simba vs mgambo shooting, u/taifa
13/4 azam vs simba, u/taifa
27/4 simba vs polisi moro, u/taifa
11/5 toto africa vs simba, ccm kirumba
18/5 yanga vs simba, u/taifa
NB: Inaweza kubadikika mda wowote
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment