Simba sc waliwakaribisha mtibwa sugar katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam wakiwa na kumbukumbu ya kupokea kichapo katika duru la kwanza toka kwa mtibwa sugar na leo kukubali kupokea kichapo cha goli 1-0.
Mtibwa sugar iliyopoteza michezo yake 3 katika uwanja wa manungu complex na kutoa sare na yanga katika uwanja wa taifa na leo kufanikiwa kuondoka na point zote tatu.
Mtibwa iliyo na ma mchanganyiko mzuri wa wakongwe na vijana goli lao lilifungwa na Selvatory Ntebi akiunga pari ya mkongwe Shaban Nditi katika dakika ya 18 na goli hilo kudumu mpaka mwisho wa mchezo.
Katika dakika ya 84 simba sc walipata pigo baada ya Juma Nyosso kuzawadiwa kadi nyekundu na simba kumaliza mchezo wakiwa pungufu kwa mchezaji mmoja.
Kwa matokeo hayo simba wamebakiwa na pointi zao 31 wakiwa nyuma kwa point 5 toka kwa azam fc na point 8 toka kwa waongoza ligi yanga.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment