VITA NYINGINE KATI YA AZAM NA MTIBWA MANUNGU

Ligi kuu xa vodacom inaendelea leo kwa mchezo mmoja kati ya Azam fc na Mtibwa sugar utakao chezwa kwenye uwanja wa Manungu complex.

Azam walitu Morogoro jana na kikosi kizima cha wachezaji 25 pamoja na viongozi 8 teyari kwa mchezo huo mgumu kwa pande zote mbili.

Wenyeji Mtibwa sugar wakitokea kwenye kutoa sare na yanga wapo katika nafasi ya 7 wakiwa na point 23 wakati wapinzani wao azam fc wapo katika nafasi ya 2 wakiwa na point 30.

Azam watakosa huduma ya beki wa kushoto Samir Hajji Nuhu aliyemajeruhi, huku wakichachiwa na urejeo wa washambuliaji John Bocco na Kipre Tchetche waliokosa michezo miwili ya awali kutokana na majeraha.

Mtibwa sugar iliyokusanya wachezaji wakongwe na chipukizi wao hawana mchezaji aliyemajeruhi.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana kwenye mashamba hiyo ya miwa Mtibwa sugar waliwafunga Azam fc goli 1-0, wakati mchezo wa mwisho kukutana azam fc waliibuka na ushindi mchezo uliochezwa visiwani Zanzibar mapema mwaka huu katika mchezo wa kombe la mapinduzi.

Azam na mtibwa wamekuwa na mvutano na kuwa na soka zuri kila wanapo kutama na ni miongoni mwa michezo migumu kuitabiri.


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.