Vita kubwa katika mchezo wa kesho utakuwa katika eneo la kati ya uwanja inayoundwa na wachezaji Michael Bolou, Salum Aboubakar 'Sure boy' na Humphrey Mieno kwa upande wa azam na Athumani Iddi 'Chuji', Franky Domayo na Haruna Niyonzima 'Fabrigas' kwa upande wa yanga.
Azam kesho itakuwa na nyota wake wote ukiwaondoa Uhuru Selemani na Samir Haji Nuhu walio majeruhi, huku Kipre Bolou na Brian Umony walio umia katika mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya al-nasri, wakirejea kuwakabili yanga.
Wakati yanga wakiwa na kikosi kamili ambacho hakikuwa na mchezo wowote wa ushindani toka february 13 walipo wachapa African lyon goli 4-0, wakati wapinzani wao azam wakitokea kuwachapa jkt ruvu goli 4-0 february 20.
Kocha wa azam fc Stewart Hall amesema kuwa urejeo wa Umonyi na Bolou ni chachu kwa wachezaji wengine kuelekea mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom.
Kocha wa yanga amesema kuwa azam ni timu nzuri na ni matumaini ya mchezo kuwa mgumu na ni vigumu kuutabiri.
Azam na yanga zote zinapoint 36 yanga ikiizidi azam katika uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa, huku azam wakiwa mbele kwa mchezo mmoja.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment