vilabu

MBEYA CITY KUWAKABILI KIMONDO KESHO BADALA YA MTIBWA SUGAR

Mechi ya kirafiki iliyokuwa ichezwe kesho jumapili katika wilaya ya Kyela kati ya Mbeya city fc na Mtibwa sugar haito kuwepo tena, kutokana na Mtibwa sugar kushindwa kufika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye kurasa ya Mbeya city FC inaeleza kuwa vinara wa ligi kuu ya vodacom Mtibwa sugar wameharbikiwa na gari.

"Mechi ya kirafiki kati ya Mbeya city fc na Mtibwa sugar fc iliyokuwa ifanyike wilayani Kyela hapo kesho haitakuwepo baada ya timu ya Mtibwa fc kuharibikiwa na gari hivyo kushindwa kuwasili jijini Mbeya", ilieleza taarifa hiyo katika ukurasa wa Mbeya city.

Kutokana na kutokuwepo kwa mchezo huo, Mbeya city wamepanga kucheza na Kimondo fc inayoshiriki ligi daraja la kwanza hapo kesho.

"Timu ya Mheya city kesho itacheza na timu ya Kimondo ya Mbozi katika mji wa Viwawa hii na katika kujiandaa na ligi kwa timu zote mbili, Kimondo inashiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara." ilihitimisha taarifa ya Mbeya city katika ukurasawao wa facebook.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.