Thomas Ulimwengu akijaribu kumtoka mchezaji wa Malawi |
Katika mchezo wa marejeano hii leo Malawi waliibuka na ushindi wa goli 1-0, mchezo uliochezwa nchini Malawi na kufanya Taifa stars kuibuka na ushindi wa goli 2-1 baada ya ushindi wa goli 2-0 katika mchezo wa awali uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo wa leo Malawi waliuwanza kwa kasi kwa dhamira ya kupata goli la mapema kitendo kilichopelekea kukosekana kwa utulivu kwa upande wa Taifa stars na kupelekea Stars kucheza mchezo wa kubutua.
Katika kipindi cha kwanza Stars walipata nafasi moja kupitia kwa Thomas Ulimwengu ambapo aliipoteza nafasi hiyo huku Malawi wakitengeneza nafasi kadhaa ambapo kipa Ally Mustafa akishirikiana vyema na safu yake ya ulinzi yaliyazima.
Katika dakika ya 43 John Banda aliiandikia Malawi goli pekee katika mchezo wa leo kwa shuti la nnje kidogo ya eneo la hatari na mpira kumshindwa kipa Ally Mustapha.
Kipindi cha pili kilianza kwa Said Hamisi Ndemla kumpisha John Bocco mabadiliko yaliyo pelekea Stars kuanza kipindi cha pili tofauti na kipindi cha kwanza na kufanikiwa kufika langoni mwa Malawi mara kadhaa.
Katika dakika ya 74 aliingia Mrisho Ngassa kuchukuwa nafasi ya Faridi Mussa Maliki mabadiliko yaliyopelekea Malawi kupunguza mashambulizi langoni mwa stars ns mpaka mchezo unamalizika Malawi goli 1 Tanzania hawajapata kitu.
Kwa matokeo hayo ya leo yanapelekea Tanzania kufuzu kwa hatua inayo fuata kwa matokeo ya jumla ya goli 2-1, na hatua inayo fuata watakutana na Al-geria.
Taifa stars leo: Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Kelvin Yondan, Nadir Haroub, Himid Mao, Mudathir Yahya, Said Hamisi Ndemla/John Bocco 45', Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, Farid Mussa Maliki/Mrisho Ngassa 74'a
0 comments:
Post a Comment