
Simba SC alikuwa mgeni wa Azam FC katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex, na kumalizika kwa sare ya bila kufungana na kupelekea kila timu kufikisha point 4.
Katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Sokoine Mbeya, Tanzania Prisons walianza kwa kuandika goli la kwanza katika dakika ya 4 kupitia kwa Rashid kabla ya Majimaji kusawazisha katika dakika ya 8 kupitia kwa Luheza na kupelekea mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.
Katika dakika ya 64 Rashid aliandikia prisons goli la pili liliodumu mpaka dakika ya 90 baada ya Majimaji kusawazisha kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Luheza na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2 na kuifanya Prisons kufikisha pointi sawa na Azam na Simba lakini Simba wanakuwa kileleni kwa uwiano mzuri wa nagoli ya kufunga na kufungwa.
0 comments:
Post a Comment