Mabingwa wa kombe la shirikisho Simba SC wamekwama kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya vodacom baada ya leo kwenda sare ya goli 2-2 na Mbao FC mchezo uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba hiii leo.
Simba SC waliuwanza mchezo wa leo kwa kasi na kufanikiwa kupata goli la kuongoza kupitia kwa Shiza Kichuya katika dakika ya 16 akimalizia krosi ya Erasto Nyoni na kupelekea kipindi cha kwanza kumalizika kwa simba sc kuwa mbele kwa goli 1-0.
Katika kipindi cha kwanza kulifanyika mabadiliko mawili ambapo Mbao FC walikuwa wa mwanzo kwa kumpumzisha Hebert Lukindo na kuingia Said Said katika dakika ya 39, huku Simba SC wakimtoa Shiza Kichuya na nafasi yake kuchukuliwa na Haruna Niypnzima katika dakika ya 45.
Katika dakika ya 46 Mbao FC walisawazisha goli kupitia kwa Habibu Haji kabla James Kotea kuifungia Simba SC goli la pili katika dakika ya 48 akiunga mpira wa faulo uliopigwa na Erasto Nyoni.
Mbao FC walisawazisha goli hilo katika dakika ya 83 kupitia kwa Boniface Maganga na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
Matokeo ya mchezo huo inaifanya Simba SC kufikisha pointi 8 katika michezo 4 waliyoicheza wakiwa nyuma kwa pointi moja kwa vinara Mtibwa wenye pointi 9 katika michezo mitatu huku Azam FC akiwa nyuma ya Simba SC wakiwa na pointi 7 katika muchezo 3.
0 comments:
Post a Comment