Mlowe: Unaswali kuhusu Uncle
Mrisho Khalfan Ngassa ni miongoni mwa wachezaji wachache wa Tanzania walio onyesha kiwango chake katika michuano ya CECAFA Tusker Chalenji Cup yanayo itimishwa leo katika uwanja wa Taifa kwa mchezo baina ya Rwanda na Uganda.
Kutokana na uwezo aliouonyesha kumempelekea bwana Raymond Mlowe kuweka post katika ukurasa wa Kandanda ambapo Kitaa umeutembelea.
TWENDE KITAANI
Raymond Mlowe
MRISHO KHALFAN NGASSA 'UNCLE'...Je, Kuna maswali?
Fernandes Ndenje:
Mengi sana
Ally Suru:
Kwanini anaendelea kucheza soka nchini?
Fernandes Ndenje:
Mpira ule wa kukimbiza, ndo coach kamfundisha au kipaji maalum?
Frank Robert Rweyemamu:
Hahahaha..hajawah kufundishwa yule Ndeje.. Kwa hiyo usishangae.
Raymond Mlowe
Ally Suru...Swali lako lihifadhi hadi february 2012 (rejea taarifa toka Settle Sounders)....Fernandes...anacheza kulingana na mechi pamoja na maelekezo ya coach, ofcourse kipaji cha kukimbia amejaliwa (ni credit kwa soka la kisasa).
Frank mmh! Kazi ya Micho hiyo!
Frank Robert Rweyemamu:
Hahahaaa...yule hajafundishwa kaka....me mwenyewe c kocha tu ila kwa upeo wangu mdogo naona mapungufu mengi sana. Huwa nina msemo wangu kuwa "Uncle" ni zaidi ya Lennon na Walcott, sema yeye hajapata exposure tu kipindi ilichokuwa anatakiwa kufundishwa mpira....
Na hilo c kwa Ngassa tu, bali ndo kilio changu kwa wachezaji wote wa nchini. Usishangae sasa hivi tunatafuta mchawi kila kukicha, ila mchawi wetu ndo huyo....
Silla Yalonde:
Very true Frank, kuna umri ambao mchezaji ni rahisi sana kupokea vitu vingi vya kiufundi toka kwa mwalimu haswaa akiwa ktk umri mdogo, hizi technical issues humkaa mchezaji na huendelea kucheza huku akikua nazo kichwani, na zipo BASIC ambazo hazibadiliki ila sasa nyingine zinakuwa applied kutokana na mazingira au mechi! wachezaji wetu weng wao wako very talented lakini hawana knwoledge ya kutosha ambayo itawafanya waapply skills zao kwa wakati muafaka! Tuna tatizo kubwa la mfumo wa programu za soka la watoto na vijana kwa ngazi ya vilabu na taifa...tukifanikiwa hapo basi tutaongelea mambo makubwa ya soka zaidi ya hao wa Afrika magharibi na Waarabu..
Frank Robert Rweyemamu:
Yah Silla, thats wat am talking about kaka! Lack of 'Game knowlege' na 'Technical competency' ndo wachawi wetu wakubwa.
Raymond Mlowe
Game na Uganda niliona jamaa alijitahidi sana katika suala la technical competency, pia kuna ile game na Wapalestina mwaka ule, labda makosa aliyonayo ni ya 'Game knowledge' zaidi.
Cheki mjadala mzima katika Kandanda
0 comments:
Post a Comment