MECHI YA NGORONGORO HEROES YAINGIZA MIL 12/-
Mechi
ya kwanza ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika
kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro
Heroes) na Nigeria (Flying Eagles) iliyochezwa juzi (Julai 29 mwaka huu)
imeingiza sh. 12,901,000.
Fedha
hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 3,377 waliokata tiketi
kushuhudia pambano hilo lililochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Sehemu
iliyoingiza watazamaji wengi ilikuwa viti vya bluu na kijani ambapo
2,697 walikata tiketi kwa kiingilio cha sh. 3,000 kila mmoja. Viingilio
vingine katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya
chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B, na sh. 15,000 kwa VIP A iliyoingiza
watazamaji 21.
Mgawanyo
wa mapato hayo ni kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) ilikuwa sh. 1,967,949.15, gharama ya kuchapa tiketi sh.
2,250,000, gharama za waamuzi na kamishna wa mechi hiyo sh. 760,000 na
ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000.
Malipo
kwa Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000, asilimia 20 ya
gharama za mchezo ni sh. 714,610.17, asilimia 10 ya uwanja sh.
357,305.08, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh.
178,652.54 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
sh. 2,322,483.05.
Mechi
ya marudiano ya michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani
nchini Algeria itachezwa Agosti 12 mwaka mjini Ilorin, Jimbo la Kwara,
Nigeria.
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA SIREFA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida (DOREFA) uliochaguliwa katika
uchaguzi uliofanyika Julai 28 mwaka huu.
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa SIREFA walivyo na imani kubwa kwao katika
kusimamia mchezo huo mkoani Singida.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya SIREFA
chini ya uenyekiti wa Baltazar Kimario ambaye amechaguliwa kwa mara ya
kwanza.
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha
shughuli za mpira wa miguu mkoani Singida kwa kuzingatia katiba ya
SIREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya SIREFA na Kamati ya Uchaguzi
ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za
uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliofanyika Chuo Cha Maendeleo ya
Jamii Singida ni Baltazar Kimario (Mwenyekiti), Hussein Mwamba (Katibu
Mkuu), Gabriel Gunda (Katibu Msaidizi), Gabriel Mwanga (Mhazini), Hamisi
Kitila (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Omari Salum (Mwakilishi wa Klabu
TFF), Yagi Kiaratu na Dafi Dafi (wajumbe wa Kamati ya Utendaji).
Nafasi
za Makamu Mwenyekiti, Mhazini Msaidizi na wajumbe wawili wa Kamati ya
Utendaji zitajazwa katika uchaguzi mdogo utakaofanyika baadaye.
MICHELSEN AITA 22 KAMBI YA COCA-COLA
Kocha
wa timu za Taifa za vijana za Tanzania, Jakob Michelsen ameita
wachezaji 22 kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya Coca-Cola
itakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Baadaye
watachujwa na kubaki 16 ambao ndiyo watakaokwenda kwenye michuano ya
Afrika Kusini. Wachezaji waliochaguliwa wametokana na michuano ya Copa
Coca-Cola iliyofanyika jijini Dar es Salaam na mkoani Pwani kuanzia Juni
24- Julai 2 mwaka huu.
Wachezaji
walioitwa ni Abdulrahman Mandawanga (Dodoma), Abraham Mohamed (Mjini
Magharibi), Ayoub Alfan (Dodoma), Bakari Masoud (Tanga), Daniel Justin
(Dodoma), Denis Dionis (Ilala), Edward Songo (Ruvuma), Fikiri Bakari
(Tanga), Hassan Kabunda (Temeke), Joseph Chidyalo (Dodoma), Mutalemwa
Katunzi (Morogoro) na Mwarami Maundu (Lindi).
Wengine
ni Nankoveka Mohamed (Ilala), Nelson Peter (Morogoro), Omari Saleh
(Singida), Rajab Rajab (Mwanza), Said Said (Kagera), Shiza Kichuya
(Morogoro), Shukuru Msuvi (Temeke), Tanganyika Suleiman (Kigoma),
Tumaini Baraka (Kilimanjaro) na William John (Ruvuma).
Pia
Michelsen ameongeza wachezaji saba kwenye kikosi cha Serengeti Boys
ambacho Septemba mwaka huu kitacheza na Kenya kuwania tiketi ya fainali
za vijana wenye umri chini ya miaka 17 za Afrika zitakazofanyika mwakani
nchini Morocco.
Wachezaji
walioongezwa kwenye kikosi hicho ambao pia wametoka kwenye Copa
Coca-Cola ni Abdallah Baker (Mjini Magharibi), Abdallah Kheri (Mjini
Magharibi), Calvin Manyika (Rukwa), Dickson Ambunda (Mwanza), Hassan
Mganga (Morogoro), Miza Abdallah (Kinondoni) na Mzamiru Said (Morogoro).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment