FDL

PANONE NA MBAO KUVUNGU SAWA, POLISI MORO IKITOA KICHAPO


Ligi daraja la kwanza inayodhamniwa na Stars times imeendelea leo kwa michezo kadhaa kuchezwa ambapo Panone FC wakitoka kupata ushindi katika mchezo wa kombe la TFF, hii leo wamebanwa vilivyo na Mbao FC.

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Ushiriki vijana wa kocha msaaidizi wazamani wa Yanga Felix Minziro, Panone FC walitoka sare ya goli 1-1 na vijana toka mkoani Mwanza Mbao FC.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo imeshuhudia Polisi Morogoro ikiibuka na ushindi wa goli 2-1 mbele ya Kimondo FC.


Matokeo ya StarTimes League:

Kiluvya 1 - 0 Mji Mkuu,
Polisi Morogoro 2 - 1 Kimondo,
Kurugenzi 3 - 1 Burkinafaso,
Panone 1 - 1 Mbao FC,
Polisi Mara 1 - 0 Rhino Rangers,
JKT Oljoro 2 -1 JKT Kanembwa

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.