FDL

RUVU SHOOTING KUSAKA POINT 1 KESHO KUREJEA VPL


TIMU ya Ruvu Shooting inahitaji pointi moja tu ili kurejea katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, wakati kesho itakapocheza na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Wambi Mafinga.

Ruvu Shooting ina pointi 28 na inahitaji pointi moja tu ili kufikisha 29, pointi ambazo hazitaweza kufikiwa na timu nyingine yoyote ya Kundi C ikiwemo Njombe Mji ambayo inaweza kufikisha pointi 28 tu hata kama itashinda mechi zake zote.

Mchezo mwingine ambao utakuwa na msisimko wa aina yake ni ule wa Gita Gold dhidi ya Polisi Tabora kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, ambapo timu yoyote itakayoshinda itajiweka katika nafasi nzuri ya kukaribia kupanda daraja. Geita wana pointi 24 huku Polisi ikiwa na pointi 21, hivyo yeyote atakayeshinda leo atazidi kujiweka vizuri.

Njombe Mji hadi sasa ina pointi 19 na kama itashinda mechi zake tatu zilizobaki, basi itafikisha pointi 28, ambazo tayari zimefikiwa na Ruvu Shooting. Ruvu Shooting iliteremshwa daraja baada ya kufanya vibaya msimu uliopita pamoja na Polisi Morogoro na Rhino ya Tabora huku Mwadui FC, Toto African, African Sports na Majimaji ya Songea.

Vita hiyo ya kupanda daraja itaendelea pia katika makundi mengi ya A na B. Leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, wenyeji Polisi Dodoma wataikaribisha African Lyon katika mchezo wa ligi hiyo huku Kiluvya United wakiwakaribisha Mji Mkuu (CDA) katika uwanja wa Mabatini Mlandizi.

Mechi zingine za leo ni Polisi Morogoro dhidi ya Kimondo FC uwanja wa Jamhuri, huku Kurugenzi ikiwakaribisha Burkinafaso kwenye Uwanja wa Wambi mjini Mafinga. JKT Mlale watawakaribisha Njombe Mji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea, Panone dhidi ya Mbao FC uwanja wa Ushirika Moshi, Polisi Mara watakuwa wenyeji wa Rhino Rangers Uwanja wa Karume mjini Musoma, huku JKT Oljoro wakiwaribisha JKT Kanembwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kwenye Uwanja wa Wambi Mafinga, Lipuli watacheza na Ruvu Shooting Uwanja wa Wambi Mafinga huku Polisi Tabora wakicheza dhidi ya Geita Gold uwanja wa Ali Hassani Mwinyi mjini Tabora. Ashanti itacheza na Friends Rangers kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Habari Leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.