TFF

Simba na Yanga ni 5000, Mbaga kusimama kati

Viingilio vya mpambano wa watani wa jadi nchini Simba na Yanga vimetajwa ambapo kiingilio cha chini ni Tsh 5000 huku chajuu kikiwa Tsh 20000, pamoja na mwamuzi atakae chezesha mtanange huo hapo oktober 29.

Taarifa toka kwa Ofisa habari wa Shirikisho la mpira Tanzania Tff, Boniface Wambura inatueleza:

WAAMUZI MECHI YA YANGA, SIMBA

Mwamuzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Oden Mbaga kutoka Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi namba 78 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Simba itakayofanyika Oktoba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi wasaidizi katika mechi hiyo ambao wote wanatambuliwa na FIFA ni Hamis Chang’walu wa Dar es Salaam ambaye atakuwa namba moja, na John Kanyenye (Mbeya) atakayekuwa namba mbili.

Mtathimini wa waamuzi (referee assessor) atakuwa Soud Abdi kutoka Arusha wakati kamishna wa mchezo huo ni Mohamed Nyange kutoka Dodoma.


VIINGILIO PAMBANO LA OKTOBA 29

Viingilio vya pambano la Yanga na Simba litakalofanyika Oktoba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom vitakuwa kama ifuatavyo;
Viti vya kijani na bluu kiingilio kitakuwa sh. 5,000,
Viti vya rangi ya chungwa ni sh. 7,000,
VIP C ni sh. 10,000,
VIP B ni sh. 15,000
VIP A ni sh. 20,000.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepanga kuuza tiketi hizo siku moja kabla ya mchezo na siku yenyewe ya mechi katika maeneo ambayo yatatangazwa baadaye.


MECHI YA KAGERA SUGAR v COASTAL

Mechi namba 89 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Kagera Sugar na Coastal Union iliyopangwa kufanyika Novemba 2 mwaka Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba imesogezwa mbele kwa siku moja.

Uamuzi wa kusogeza mechi hiyo hadi Novemba 3 mwaka huu umetokana na wamiliki wa Uwanja wa Kaitaba kuruhusu utumike kwa sherehe za Mwenge wa Uhuru.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.