Mafisango arejeshwa kundini
Kiungo wa Simba mwenye asili ya Congo DR Patrick Mutesa Mafisango amejumuishwa katika msafara wa Simba, utakaoenda nchini Algeria siku ya jumatatu ya april 2.
Mafisango aliondolewa katika kambi ya Simba wiki hii kwa kosa la utovu wa nidhamu na aliondolewa katika orodha ya wachezaji watakao safiri na timu kwenda kukabiliana na ES-Setif ya Algeri kati ya April 6-8 mwaka huu.
Mmoja wa kiongozi wa Simba akizungumza na Magic FM jioni ya leo katika kipindi cha michezo na magic alisema kuwa kikosi cha Simba kitasafiri jumatatu alfajiri kikiwa za silaha zake zote akiwemo Mafisango.
Amesema kuwa uongozi wa Simba umeamu kumsamehe kiungo huyo, ambapo ilipangwa aje asikilizwe mara baada ya timu kurejea toka Algeria na hukumu yake kutolewa wakati huo.
Simba na Es-setif wanataraji kucheza mchezo wa pili waraundi ya pili katika kombe la shirikisho CAF, ambapo mchezo wa awali uliochezwa katika uwanja wa Taifa ulishuhudia Simba wakiwachapa Es-setif goli 2-0.
0 comments:
Post a Comment