VPL

Mafisango aiweka pazuri Simba, Toto waikamata Yanga


Patrick Mutesa Mafisango

Goli la kiungo toka nchini Rwanda Patrick Mafisango lilitosha kuwapa point 3 Simba SC, wakati mpinzani wake wa jadi Yanga akilala goli 3 toka kwa Toto Africa katika muendelezo wa michezo ligi kuu ya vodacom.

SIMBA YAJIKITA KILELENI

Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Simba SC wameendelea kukalia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom, baada ya kuwachapa Ruvu Shooting goli 1-0 katika nyasi za uwanja wa Taifa na kufanya wigo wa point baina yake na Azam kuwa 3.

Simba ilibidi wangoje mpaka dakika ya 80 ndipo walipo pata goli lao la ushindi lililofungwa na Patrick Mutesa Mafisango.

TOTO AFRICA WAITOA RELINI YANGA

Kwa mara ya kwanza katika historia ya uwanja wa CCM Kirumba kushuhudia Toto Africa akiibuka na ushindi mbele ya Yanga iliyo katika mbio za kusaka ubingwa wa Tanzania Bara.

Katika mchezo huo Toto Africa waliwaduwaza Yanga baada ya kupata goli katika dakika ya 18 kupitia kwa Mussa Said na Kabla hawajakaa sawa walishangaa wanafungwa la pili kupitia kwa Kulwa Mobbi katika dakika ya 24.

Mussa Saidi alirejea kwenye nyavu za yanga katika dakika ya 39, huku yanga walipata goli lao la kwanza kupitia kwa Hamisi kiiza dakika ya 43. Na Toto kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 3-1.

Yanga walirejea kipindi cha pili na kupata goli la pili kupitia kwa Hamisi Kiiza katika dakika ya 65, likiwa ni goli lake la pili katika mchezo wa leo na kupelekea mchezo kumalizika kwa Yanga kufungwa goli 3-2 na Toto Africa.

Kocha mkuu wa Yanga Mserbia, Kosradin Papic alizomewa na mashabiki wa Yanga mjini Mwanza kutokana na kiwango kibovu ambacho timu hiyo inacheza hivi sasa.

Kwa matokeo hayo yanapelekea kutofautiana kwa point 10 na vinara Simba na point 7 kutoka kwa Azam lakini wakiwa nyuma mchezo mmoja.

MCHEZO MWINGINE

COASTAL UNION 2-4 VILLA SQUAD

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.