Mchangani

CDA YAANZA VYEMA SITA BORA DOM

TIMU ya soka ya CDA imeanza vizuri hatua ya Sita Bora ya Ligi ya Mkoa wa Dodoma baada ya kuifunga Kikuyu mabao 3-1 katika mchezo mkali uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Ligi hiyo ambayo ilianza mapema wiki hii kwa timu za Chinangali kutoka sare ya 0-0 huku Area C nao wakilazimishwa sare kama hiyo katika mechi zote zilizochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Katika mchezo uliochezwa juzi, Kikuyu ilianza kwa kucheza soka la kujiamini na walipata bao dakika ya 30 lililofungwa na Ibrahim Nyagawa kwa penalti baada ya mmoja wa washambuliaji wake kuchezewa rafu ndani ya eneo la hatari.

Baada ya bao hilo, CDA walicharuka na kuanza kulishambulia lango la Kikuyu ambapo mshambuliaji Novatus George alisawazisha dakika ya 39 baada ya kuwatoka mabeki na kupiga shuti lililokwenda wavuni.

Kipindi cha pili, CDA walionekana kutawala mchezo huo ambapo mshambuliaji wake hatari, Ally Lutavi aliwainua mashabiki wa timu hiyo baada ya kufunga bao la pili akiunganisha krosi ya Rajabu Mugarula.

Wakati Kikuyu wakitafuta namna ya kusawazisha bao hilo, walijikuta wakichapwa lingine lililofungwa tena kwa Lutavi aliyewazidi mbio mabeki na kupiga shuti hafifu lililokwenda moja kwa moja wavuni.

Pamoja na ushindi huo, kwa upande wa CDA, lakini Kikuyu ambayo ni wageni katika ligi hiyo, walionesha kandanda la kuvutia hasa kwenye kipindi cha kwanza, lakini wakaja kuzidiwa kipindi cha pili.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.