vilabu

CHIPO ATETEA KUTEMA WAKONGWE

KOCHA Mkuu wa timu ya Coastal Union, Yusuf Chipo amesema baada ya kutokea maneno kwamba timu hiyo hasa wachezaji wakongwe walicheza ovyo dhidi ya Azam FC, aliamua kubadilisha kikosi hicho kwa malengo ya kufanya vizuri kwenye mechi zilizosalia.

Coastal Union kabla ya kushinda bao 1-0 kwenye mechi ya juzi dhidi ya Simba iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, walipata kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Azam FC, kipigo ambacho kiliibua maswali mengi ndani ya timu hiyo ambayo imekuwa ikitoa upinzani katika Ligi Kuu tangu irejee katika ligi hiyo.

“Ule ulikuwa mpira, mechi ilikuwa ni ngumu ndio maana tulifungwa mabao mengi, lakini ili kufanya vizuri niliona ngoja nibadilishe kikosi na hatimaye tumeona matunda,” alisema Chipo.

Katika mechi dhidi ya Simba, kocha huyo raia wa Kenya, aliwapumzisha baadhi ya wachezaji ambao wali- kuwepo kwenye kikosi dhidi ya Azam wakiwemo Juma Nyoso, Jerry Santo na Haruna Moshi.

Kwa mujibu wa Chipo, aliamua kufanya hivyo na kuwapa nafasi wengine ili kuonesha uwezo wao na wamefanikiwa.

Alisema mabadiliko hayo yatakuwa yanaendelea katika baadhi ya mechi zilizosalia wakilenga kufanya vizuri ili kubaki katika nafasi tano bora, na kujipanga zaidi kwa msimu ujao.

Katika msimamo wa Ligi Kuu, Coastal Union imeendelea kubaki katika nafasi ya saba wakiwa na pointi 29 nyuma ya Ruvu Shooting yenye pointi 31.



CHANZO: HABARI LEO

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.