simba

COASTAL WAWACHAPA SIMBA KIMOJA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPL96oYCu4MxwZe3xq5ZSnwFxuyW45QXKDF1CBU8Q9KHoxmiCtj4RYcR9iDXxA9dRXSU7XO8J5TljDYpg5YrwShKm0OGoJA7nXLvleapTomunwsXAIjUzPyFGHDTM36XeeBQWqI2Ts_CK1/s1600/IMG_2137.JPG
Bao pekee la dakika ya 44 lililoingizwa kimiani na beki Hamadi Juma, baada ya kupokea pasi ya mwisho kutoka kwa Razak Khalfan ndilo lililopeleka kilio mtaa wa Msimbazi baada ya bao hilo kudumu mpaka dakika ya 90.

Coastal Union ambayo ilikuwa na wachezaji chipukizi ilionyesha uhai kwa dakika zote 45 za awali mpaka kupata bao dakika moja kabla ya filimbi ya mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi upande wa Simba, ambapo mshambuliaji Ramadhan Singano 'Messi' ndie pekee alionekana hatari lakini umakini wa golikipa Fikirini, alieonekana mpya machoni mwa wengi ulisaidia kuiondoa Coastal Union kichwa chini katika uwanja wa ugenini leo.

Aidha beki wa kati Yusuf Chuma aliyumia vema urefu wake kwa kuokoa mipira mingi ya juu, huku Kibacha, Hamadi na Banda wakizuia kwa nguvu kuhakikisha ngome ya wagosi inaendelea kuwa iara.

Kikosi cha leo kilichoanza dhidi ya Simba ni: Fikirini Suleiman, Hamadi Juma, Abdi Banda, Yusuf Chuma, Mbwana Kibacha, Razak Khalfan, Ally Nassor ‘Ufudu’, Behewa Sembwana, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Kenneth Masumbuko, Danny Lyanga.
Wachezaji wa akiba ni: Mansour Alawi, Ayoub Masoud, Marcus Ndeheli, Ayoub Semtawa, Mohammed Miraji, Crispian Odula, na Mohammed Kipanga.

Baadae Kocha aliwatoa Ally Nassor, Hamadi Juma na Suleiman Kassim, wakaingia Mohammed Miraji, Ayoub Masoud na Marcus Ndeheli.

Kwa matokeo hayo Coastal Union imevuna point tatu na kufikisha jumla ya point 30, na kupaa hadi nafasi ya saba ikisubiri kucheza na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu mjini Morogoro.



MATOKEO YA MICHEZO MINGINE
 AZAM FC 1-0 OLJORO JKT

RUVU SHOOTING 2-0 ASHANTI UNITED
MGAMBO JKT 1-1 MTIBWA SUGAR

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.