ZGPL

KMKM WAICHAPA KIZIMBANI

MAAFANDE wa KMKM juzi walishinda bao 1-0 dhidi ya Kizimbani katika mchezo wa ligi Kuu ya Zanzibar uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini Unguja.

Pambano hilo lililokuwa na upinzani kiasi, liliwavutia mashabiki wachache waliohudhuria.

Miamba hiyo ilikuwa ikishambuliana kwa zamu, hali iliyowafanya waende mapumziko wakishindwa kufungana. Bao hilo la pekee la KMKM liliwekwa kimiani na Hasim Ramadha kwa pasi safi iliyotolewa na Juma Mbwana.

Kwa matokeo hayo, KMKM imefikisha pointi 33 na kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo ambayo inaongozwa na Polisi yenye pointi 37.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo kwenye uwanja huo kwa maafande hao wa KMKM kuumana na Kizimbani ikiwa ni mchezo wake kiporo.


CHANZO: HABARI LEO

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.