CHAMA cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA), kimeifungia timu ya Masukuru ya Busokelo wilayani Rungwe kucheza misimu mitatu ya Ligi Daraja la Tatu Mkoa pamoja na kuishusha daraja.
Adhabu hizo pia zilizotokana na timu hiyo kutokuwa na nidhamu kwenye hatua ya makundi ya ligi hiyo iliyomalizika hivi karibuni, itakwenda sambamba na faini ya Sh 300,000.
Katibu wa Mrefa, Haroub Suleiman alisema kuwa adhabu hizo ni maazimio ya kikao cha Kamati ya Ligi ambacho pamoja na mambo mengine, kilijadili utovu wa nidhamu wa Masukuru kutofika uwanjani katika michezo yake mitatu hivyo kuzipa timu pinzani pointi za mezani.
Alisema adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni Namba 21 ya Ligi, Kifungu B na D, na kusisitiza kuwa ili timu hiyo iruhusiwe kucheza ligi yoyote, hata baada ya kushushwa daraja lazima ilipe faini hiyo.
Alisema adhabu, pia timu ya Wenda FC ya Mbeya Vijijini itatakiwa kulipa faini ya Sh 30,000 kwa kuchelewa kikao cha kabla ya mchezo wake na Ichenjezya FC ya Mbozi uliochezwa Februari 25, mwaka huu.
CHANZO: HABARI LEO
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment