timu 10 za mkoa huo kwa ajili ya kukuza vipaji vyao.
Mwenyekiti wa IDYOSA, Edwin Mloka alisema mashindano hayo yatafanyika leo kwenye Viwanja vya Magereza, Ukonga, Dar es Salaam.
Alisema timu zitakazoshiriki kwenye mashindano hayo ni Yoso FC, Double Road ya Majohe, Majohe FC, Makoba FC na Ukonga United ambazo zitakuwa kwenye Kundi A.
Kundi B ni Vumbua Vipaji, Tabata City, Cologne FC, Wakati Ujao FC na Tabata Rangers. Mloka alisema mashindano hayo yatakuwa yakifanyika mwishoni mwa wiki kutokana na wachezaji wengi kuwa ni wanafunzi, nafasi zao ni Jumamosi na Jumapili.
Alisema mashindano hayo ni utaratibu wao kwa kila mwezi ambapo huwaunga vijana mkono katika kukuza vipaji vyao.
“Ni utaratibu wetu wa kawaida kuandaa mashindano ya vijana, tumelenga kuhamasisha vijana kushiriki michezo, lakini pia, wale watakaofanya vizuri wataonekana na pengine kuwa kivutio kwenye timu nyingine,” alisema mwenyekiti huyo.
CHANZO: HABARI LEO
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment