VPL

YANGA YAMKUTA YALIYOMKUTA SIMBA MKWAKWANI, WALA MBILI MGAMBO WAKIWA PUNGUFU

Mabingwa watetezi Yanga wameshindwa kuutavuna mfupa uliomshindwa Simba SC, baada ya leo kukubali kichapo cha goli 2-1 toka kwa Mgambo shooting, wakati wapinzani wao katika mbio za ubingwa Azam FC wakiwachapa Simba SC goli 2-1.

PENATI MBILI ZA SHUHUDIWA MKWAKWANI

Katika uwanja wa Mkwakwani ulioshuhudia Yanga wakilala kwa goli 2-1, pia kulishuhudi penati mbili zikitolewa na zote zikitiwa nyavuni.

Katika mchezo huo wa leo Mgambo walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Fuluzulu Maganga katika dakika ya kwanza ya mchezo.


Katika dakika ya 30 Mbambo shooting walijikuta wakitakiwa kumaliza mchezo wakiwa pungufu baada ya Mohammed Neto kutolewa nnje kwa kadi mbili za njano, huku kipa wa Mgambo shooting Salehe Tendega akishindwa kumailizia mchezo baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na kipa Tony Kavishe katika dakika ya 32.

Mpaka timu hizo zina kwenda mapumziko Mgambo Shooting iliyo ifunga Simba SC katika uwanja huo wa Mkwakwani walikuwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kusaka goli la kusawazisha ambapo walifanikiwa kulipata katika dakika ya 53 kupitia kwa nahodha wa Yanga Nadir Haroub kwa mpira wa penati iliyotokana na beki wa mgambo kuunawa mpiria katika eneo la hatari.

Wakati yanga wakisaka goli lingine la pili walijikuta wkaiwazawadia Mgambo mkwaju wa penati na kutiwa wafuni na Busungu katika dakika ya 65, na kupelekea Mgambo kumaliza mchezo wakiwa mbele kwa goli 2-1.

UWANJA WA TAIFA, AZAM WAONGEZA TOFAUTI YA POINTI
 
Azam FC leo wameendeleza dhamira yao ya kutaka kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara baada ya leo kuwafunga Simba SC goli 2-1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa.

Azam FC iliandika goli lake la kwanza kupitia kwa Hamisi Mcha Viali katika dakika ya 17 kabla ya Joseph Owino aliyepata kuitumikia Azam FC  kipindi cha nyuma kuisawazishia Simba SC katika dakika ya 45 na kupelekea mchezo kwenda mapumziko wakiwa sre ya goli 1-1.

Katika kipindi cha pili Azam FC walirejea kwa kasi huku wakisaka goli la ushindi lililofungwa nanahodha John Bocco kwa kichwa akiunga mpira uliogonga mwamba kufuatia shuti la Kipre Hermani Tcheche.

Goli la John Bocco liliihakikishia Azam FC ushindi wa goli 2-1 na hivyo kujikusanyia pointi 53 baada ya kucheza michezo 23 na kuiwacha Yanga wakibakiwa na pointi zao 46 baada ya leo kukubali kichapo cha goli 2-1 baada ya kucheza michezo 22.

Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Aggrey Morris, David Mwantika, Kipre Balou, Himid Mao/Bryson Raphael dk75 , Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’, Kipre Tchetche/Brian Umony dk80 na Khamis Mcha ‘Vialli’/Kevin Friday dk55.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.