
Faru Jeuri leo walikuwa wanachuana na Kauzu FC ya Tandika katika mchezo wa fainali wa kombe la Sports extra na kufanikiwa kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya penati 4-3.
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Bandari, ulishuhudia dakika 90 zikimalizika kwa sare ya bila kufnngana na mshindi kuamuliwa na mikwaju ya penati.
Katika dakika 90 za mchezo Kauzu na Faru jeuri walikuwa wanatawala mchezo kwa kupokezana na kila mmoja kupoteza nafasi kadhaa japo Kauzu FC ndio waliopoteza nafasi ya wazi zaidi katika kipindi cha kwanza.
Kwa matokeo hayo ya mikwaju ya penati Faru jeuri wakishiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo wamefanikiwa kuwa mabingwa wa pili wa michuano hiyo, baada ya mwaka jana kombe kuchukuliwa na Abajalo ya Sinza.
Wakati Faru jeuri wakiwa mabingwa wapya wa masjindano hayo, kikundi cha ushangiliaji cha Kauzu FC ndio waliokuwa kikundi bora cha ushangiliaji katika michuano ya mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment