![]() |
mfungaji wa goli la kusawazisha la yanga, Andrew Countinho |
Katika mchezo wa leo Mbeya city walikuwa wa mwanzo kuona nyavu za yanga kupitia kwa Bakari Mwinjuma'Neymar' katika dakika ya 8 ya mchezo.
Goli hilo lilidumu kwa dakika 8 kabla ya Andrew Countinho kuisawazishia Yanga SC katika dakika ya 16 ya mchezo, huku Amisi Tambwe akiipeleka yanga mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2 baada ya kuifungia yanga goli la pili katika dakika ya 44.
Katika kipindi cha pili mshambuliaji mpya wa yanga toka Zimbabwa Wilbert Ngoma aliiandkika yanga goli la 3 katika dakika ya 52 ya mchezo kabla ya Meshack kuiandikia goli la pili Mbeya city katika dakika za lala salama na kupelekea mchezo kumalizika kwa yanga kuibuka na ushindi wa goli 3-2.
Huo ni ushindi wa tatu kwa yanga katika michezo mitatu ya kirafiki waliyocheza jijini Mbeya, ambapo walianza kwa kuifunga Mbaso Academy goli 4-1, na kisha kuifunga Tanzania Prisons goli 2-1 na leo kuhitimisha kwa goli 3-2.
Yanga imeweka kambi jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam Fc mchezo utakao chezwa wikiendi ijayo katika uwanja wa Taifa, huku kukiwa na taarifa ya yanga kurejea jijini kesho kumalizia maandalizi yao ya mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment