VODACOM WATAKA USHINDANI WA KWELI, WEBSITE YA VPL HII HAPA

Wakati mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom 2012/13 ukitarajiwa kuanza jumamosi hii (january 26), wadhamini wa ligi hiyo wamesema wanataka kushuhudia ligi yenye ushindani zaidi, huku kukizinduliwa website (mtandao) wa ligi hiyo.

Wadhamini hao wa ligi kuu ya Tanzania bara wamesema leo jijini Dar es salaam wanataka kushuhudia mzunguko wa pili wenye ushindani wa kweli huku wakitaka kutoshuhudia upangaji wa matokeo katika duru hilo la pili.

Wakati vodacom wakisema hayo, mtandao (website) itakayo kuwa inazungumzia ligi kuu ya Tanzania bara imezunduliwa, ambayo ni www.ligikuu.co.tz

Website hiyo itakuwa na taarifa na matukio yanayohusiana na ligi kuu ya Tanzania bara.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.