BAUSI KUKWAMA TENA MBELE YA WAKENYA LEO?

Kocha wa Miembeni na aliyekuwa wa Zanzibar heroes Salum Bausi leo anataraji kuiongoza Miembeni kuikabili Turker ya Kenya katika nusu fainali ya kwanza ya kombe la mapinduzi ikiwa ni mwezi tu toka ashuhudie kikosi chake cha Zanzibar heroes kikitolewa na Kenya katika nusu fainali ya kombe la chalenge yaliyofanyika jijini Kampala Uganda.

Bausi alitolewa katika michuano ya chalenge kwa mikwaju ya penati na Kenya, na leo usiku atapata fursa ya kulipa kisasi katika ngazi ya vilabu, pale timu pekee ya visiwani iliyosalia katika mashindano Miembeni itakapo wakabili wakenya pekee katika mashindano hayo Tusker.

Tusker imefikia hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kuongoza kundi A wakati miembeni wakitokea kundi B wakiwa wa pili

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.