Coastal union ya Tanga walipambana na Mtibwa sugar ya Morogoro katika mchezo wa awali na kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Katika mchezo huo mtibwa sugar walimaliza pungufu kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa beki mkongwe Salum Swedi mwishoni mwa kipindi cha kwanza.
Pamoja na kuwapungufu Mtibwa sugar walikuwa wa mwanzo kuliona goli la coastal union kupitia kwa Ally Mohamed katika dakika ya 68 na coastal tnion kufanikiwa kusawazisha katika dakika ya 81 kupitia kwa nahodha Jerry Santos.
Katika mchezo wa pili uliwakutanisha makocha wazamani wa Zanzibar heroes walio fanikisha kuifikisha nusu fainali ya chelenge cup Salum Bausi wa miembeni na Stewart Hall wa azam fc na kushuhudia makocha wote wakitolewa kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumzonga mwamuzi wakati timu zikielekea mapumzikoni.
Katika mchezo huo vijana wa Bausi, Miembeni walhshindwa kufurukuta na kujikatia tiketi ya kutinga nusu baada ya kukubali kichapo cha goli 3-1 toka kwa Azam fc.
Azam walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 2 kupitia kwa mkenya Juackin Akudo akiunga kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Humphrey Mfuno.
Goli hilo halikudumu kwani katika dakika ya 4 Adeyoum Saleh aliisawazishia miembeni kwa mpira wa kona uliotinga moja kwa moja nyavuni kabla ya Gaudency Mwaikimba kuipatia goli lapili azam katika dakika ya 34 na Uhuru Seldmani kuhitimisha katika dakika ya 87.
Kwa matokeo ya jana Azam wanaongoza kundi kwa kuwa na point 4 wakifuatiwa na Miembeni wenye point 3, Coastal union wakiwa na 2 na Mtibwa sugar wenye point moja.
0 comments:
Post a Comment