kitaa

Muundo wa Kampuni wa ligi kuu

Mjadala wa kampuni na kamati wazidi kupanda kasi, huku vilabu wakifungua Facebook group inayoenda kwa jina la Ligi Kuu Tanzania, ikiwa na dhamira ya kukusanya mawazo ya wadau kuelekea kwenye kampuni.

Kitaa kimetembelea kwenye group hilo na kukutana na doc iliyoandikwa na mmoja waliopewa jukumu la kuhakikisha kampuni inaanza na inafanya kazi vyema PATRICK KAHEMELE 'PK', inayoelezea muundo wa kampuni.


TWENDE KITAANI


Muundo wa kampuni ya ligi Kuu

1. Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Ligi kuu TPL atakuwa kiongozi wa Juu wa Klabu iliyoshinda ubingwa Ligi Kuu msimu uliotangulia


2. Makamu wenyeviti watatu wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya ligi kuu TPL ni (viongozi wa juu wa timu mbili zilizoshika nafasi ya pili na tatu na Makamu wa pili wa Rais TFF anayewakilisha vilabu


3. Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Ligi kuu inahusisha wenyeviti au wakurugenzi au kiongozi wa juu wa vilabu vyote 14 (16) vinavyocheza ligi kuu, (kila klabu itatoa mjumbe mmoja).

TFF pia itakuwa na hisa kwenye kampuni ya ligi kama klabu na itakuwa na mjumbe mmoja kwenye bodi ya wakurugenzi wa kampuni.

Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya ligi ambao hawatapiga kura ni pamoja na Mjumbe mmoja toka chama cha wanasoka wa kulipwa, chama cha waamuzi FRAT, chama cha makocha TAFCA na Wadhamini wa ligi kuu


4. Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya ligi inapaswa kukutana wiki ya mwisho ya mwezi July (kabla ligi haijaanza) na wiki ya mwisho ya mwezi Januari (kabla raundi ya pili haijaanza )kila mwaka


5. Wajumbe wa kamati tendaji wa kampuni ya ligi inahusisha angalau kiongozi mmoja wa kila timu inayoshiriki ligi kuu, mwakilishi kutoka shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, chama cha makocha, chama cha waamuzi, na wawakilishi toka kwa wadhamini ambao hawatakuwa na nguvu ya kupiga kura.

Wajumbe wa kamati hizi wanapaswa kukutana angalau kila baada ya miezi miwili.


6. Kamati kuu ya TPL inahusisha Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TPL, Makamu wenyeviti wa bodi ya wakurugenzi wa TPL, na wajumbe watatu watakaochaguliwa na bodi ya wakurugenzi.

Kazi kuu ya kamati kuu ya TPL ni kuhakikisha sera zilizopitishwa na TPL zinatekelezwa na secretariet ya TPL.


7. Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya TPL itahusisha mameneja na makocha wakuu wa vilabu vyote vinavyocheza ligi kuu na Mkurugenzi wa ufundi TFF kama wapiga kura sambamba na Mwakilishi wa chama cha makocha, na chama cha wachezaji wa kulipwa ambao hawatapiga kura.


8. Kutakuwa na kamati huru ya nidhamu na rufaa ambayo itateuliwa na Bodi ya wakurugenzi ya TPL kila mwaka.

Maamuzi ya kamati hii yatapaswa kutekelezwa na klabu zote zinazoshiriki ligi kuu lakini yanaweza kupigwa kwenye kamati ya nidhamu na Rufaa ya TFF.
SOMA ZAIDI

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.