BREAKING NEWS: ZFA YAWARUDISHIA WACHEZAJI PESA ZAO

Mwakilishi wa Sports In Bongo toka visiwani Zanzibar Ally Mohamed ameripoti katika ukurasa wake wa facebook kuwa wachezaji wa Zanzibar heroes waliorejesha hela ya ushindi wa tatu waliopata katika michuano ya chalenge wamerejeshewa fedha zao na ZFA leo mchana.

Wachezaji wa Zanzibar heroes waligawana na zawadi ya mshindi wa tatu katika kombe la chalenge iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana jijini Kampala Uganda kitendo kilicho wakera chama cha soka cha Zanzibar ZFA na kuwataka wachezaji kurejesha pesa hizo na wale waliokaidi walitishiwa kufungiwa.

Taarifa iliyo naswa na Ally zinasema wachezaji waliorejesha pesa hizo wamerejeshewa pesa hizo.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.