KAGERA NA TOTO WADODA UGENINI,

Timu za kanda ya ziwa Kagera sugar ya Kagera na Toto Afrika ya Mwanza wameendelea kudoda ugenini baada ya kukubali kupokea kichapo cha pili mfululizo katika viwanja vya Arusha na Dar es salaam.

Kagera baada ya kupoteza mchezo Chamanzi leo wamepoteza tena kwa Oljoro JKT katika uwanja wa Sh. Amri Abeid uliopo jijini Arusha.

Katika mchezo huo ulioshuhudia mvua ikinyesha wakati mchezo ukiendelea, Kagera sugar wamelala kwa goli 2-0 mbele ya maafande hao wa kujenga taifa toka Arusha.

Magoli ya Oljoro yametiwa kimiani na kiungo Paulo Nongwa katika dakika ya 40, baada ya kuwalamba chenga mabeki wa kagera sugar na kuachia fataki lililo mshinda mlinda mlango wa Kagera sugar.

Goli la pili la Oljoro lilifungwa na mkouea bench Saleh Iddi aliyeingia uwanjani katika dakika ya 84 na dakika ya 87 kuifungia oljoro goli la pili.


Wakati Kagera wakipokea 2 jirani zao Toto Africa wamepokea 3 toka kwa azam fc mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam complex uliopn Chamanzi na kusiuhudiwa na kocha wa taifa stars Kim Poulsein anaetarajia kutangaza jeshi lake hapo kesho.

Katika mchezo huo azam waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 9 kupitia kwa Kipre Bolou na ilichukuwa dakika 11 kwa Brian Umony kuiandikia goli la pili azam na kuipeleka azam mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Hamphrey Meno aliipatia azam goli la 3 katika dakika ya kwanza kipindi cha pili kabla ya Suleiman Kibota kuiandikia goli la kufutia machozi katika dakika ya 77 na kupelekea mchezo kumalizika kwa azam kushinda goli 3-1.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.