Taifa stars wanataraji kuwavaa Cameroun katika kalendaya FIFA (FIFA DATE) february 6 mwaka huu katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kuanzia saa 11 jioni.
Hii itakuwa fursa nyingine kwa mapacha watatu wapinzani (Salum Aboubakary, Franky Domayo na,Mwinyi Kazimoto) kuendeleza kudhihirish ubora wao mbele ya viungo wanao tambulika na wapenzi wa soka duniani, baada ya kufanya hivyo kwa kina Yahya Touretoka Ivoqy coast, akaja Katongo na wenzake wa Zambia sasa ni zamu ya Alexs Song anaekipiga Barcelona pale watakapo ambatana na timu ya taifa ya Cameroun.
Mataifa mbalimbali nnje ya Cameroun na Rwanda walio omba kucheza na Taifa stars katika siku hiyo ya FIFA, ambazo ni Swaziland waliotaka mchezo ufanyike taifa, Congo Brazaville na Ehuiterial Gunei walitaka taifa stars wawafuate.
Mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Cameroun utawaongezea uzoefu viungo hao pacha ambao bado damu inachemka kabla ya kukutana na Morocco kathka mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza kombe la dunia nchini Brazil.
Kikosi cha Cameqoun kinachoundwa na nyota wanaosakata soka barani ulaya kinatarajia kuanza kutua february 3.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment